Home KILIMO Wakulima wa viungo washauriwa kuongeza uzalishaji

Wakulima wa viungo washauriwa kuongeza uzalishaji

0 comment 108 views

Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi ametoa wito kwa wakulima wa mazao ya viungo nchini kuzalisha kuwa wingi ili kukuza uchumi wa nchi na kujiongezea kipato. Mwinyi amesema hayo alipotembelea maonyesho ya 42 ya biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba na kuongeza kuwa, mazao hayo ikiwemo ndimu, limao, karafuu na mwani yanapotea katika soko kila siku licha ya kuwa na umuhimu mkubwa katika kuchangia uchumi wa taifa.

“Nilikuwa sijawahi kuona mwani, nilikuwa sijui mwani ni nini na una faida gani kimwili na kiuchumi lakini leo nimeelewa” Alisema Rais Mwinyi.

Ziara ya Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi katika maonyesho hayo iliambatana na uzinduzi wa siku maalum ya zao la mwani linalolimwa visiwani Zanzibar. Alisema kuwa amevutiwa na zao hilo linalolimwa zaidi visiwa vya Zanzibar na ni la nne kwa ukanda wa Afrika Mashariki likiwa pia linatumika kuzalisha mafuta ya kula. Mwinyi pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wakulima wanaozalisha mazao hayo kuzalisha kwa wingi walau hata tani 23 kwa mwaka.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Zanzibar Amina Salum Ally amesema, zao la mwani linazalishwa kuanzia tani 15 hadi 16 kwa mwaka huku watumiaji wa zao hilo wakifikia asilimia 25.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter