Katibu Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwekezaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa amewasahuri wahitimu kugeukia sekta ya kilimo na kuangalia uwezekano wa kujiajiri hususani kwenye biashara kupambana na changamoto ya ajira. Beng’i ametoa wito huo wakati akifungua semina kwa wahitimu wa shahada za jinsia na maendeleo kutoka Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Tunafahamu zipo changamoto kwenye soko la ajira hasa kwa wasomi kama nyinyi ndio maana tunahimiza utaratibu wa kujiwekea akiba na kuanzisha vikundi vya uzalishaji mali kwani mifuko mingi huwafikia watu kwa njia hii” Ameeleza Beng’i.
Katibu Mkuu huyo amewataka wasomi kujiunga kwenye vikundi wakiwa na wazo la kutekeleza ambalo litawawezesha kuomba fedha katika mifuko mbalimbali inayowasaidia vijana na kuwashauri kutumia vyema fursa zilizopo kwenye mifuko ya uwezeshaji na kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba.