Home BIASHARA Tamida yatoa neno kwa serikali

Tamida yatoa neno kwa serikali

0 comment 188 views

Chama cha wanunuzi na wauzaji wa madini Tanzania (Tamida) kimetoa wito kwa serikali kutoa elimu kwa wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite juu ya matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kuongeza uzalishaji. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamida  Sammy Mollel huku akiongeza kuwa bila kufanya hayo mrabaha wa serikali utaendelea kushuka licha ya serikali kujenga ukuta mkubwa wa kuzuia utoroshwaji wa madini katika mgodi wa tanzanite Mirerani.

Katika machimbo ya Tanzania kwa sasa kuna migodi 570 iliyopewa  leseni na kati ya hiyo ni migodi 216 pekee ndio imekuwa ikifanya kazi kwa muda wa miezi sita huku idadi ya wafanyakazi wa migodi hiyo ikiwa ni zaidi ya 5000.

Akizungumzia kuhusu uzalishaji, Mollel amesema kumekuwepo na kushuka kwa kazi kwa mrabaha wa serikali kutoka Sh. 444 milioni hadi Sh. 40 milioni kutokana na migodi mingi kusimamisha shughuli zake za uchimbaji madini.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha wachimaji Mkoani Manyara, Sadick Mnenei amesema kuwa gharama za uchimbaji na mazingira ya kuchimba tanzanite yameendelea kuwa magumu kila kukicha ikiwa ni matokeo ya kutotumia teknolojia bora ya uchimbaji sambamba na kuweka mazingira safi kwa wachimbaji wadogo wadogo.

“Migodi mingi imekwenda chini zaidi ya kilomita moja na wengi hawajapata madini, wametumia gharama kubwa baadhi wameuza nyumba wengine wanafilisiwa na mabenki sasa ili kuokoa hali hii lazima serikali ifanye upya utafiti wa madini Mirerani” Ameeleza Mnenei.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter