Home BIASHARA Mfumuko wa bei wapungua

Mfumuko wa bei wapungua

0 comment 88 views

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo ametangaza kuwa, mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Julai umepungua hadi kufikia asilimia 3.3 ikilinganishwa na asilimia 3.4 ya mwezi Juni, mwaka huu.

Kwesigabo amefafanua kuwa kupungua kwa mfumuko wa bei kunadhihirisha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Julai mwaka huu imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwa kwa mwaka ulioishia Juni mwaka huu.

“Baadhi ya bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya Julai mwaka jana na Julai mwaka huu, ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 9.5, mtama kwa asilimia 17.8, unga wa mihogo kwa asilimia 14.1, matunda jamii ya machungwa kwa asilimia 22.2, maharage kwa asilimia 5.8 na mihogo mibichi kwa asilimia 12.5,” Amesema Kwesagabo.

Kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Uganda mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 3.1 kutoka asilimia 2.2 kwa mwaka unaoishia mwezi Juni mwaka huu. Kwa upande wa Kenya, mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 4.35 kutoka asilimia 4.28 kwa mwaka ulioshia Juni.

NBS ni taasisi pekee yenye wajibu na mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa takwimu rasmi nchini ikiwa ni pamoja na takwimu za mfumuko wa bei kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau wa takwimu nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter