Home BENKI Benki ya Maendeleo kuwezesha wajasiriamali

Benki ya Maendeleo kuwezesha wajasiriamali

0 comment 104 views

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo Ibrahim Mwangalaba amesema benki hiyo imejipanga kuhudumia wajasiriamali wadogo ili kuwapa fursa ya kukuza mitaji yao na kuwawezesha kuingia katika biashara kubwa ya kuanzisha viwanda. Mwangalaba amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya utendaji kazi wa benki hivyo na kueleza kuwa, benki ya maendeleo imekuwa mstari wa mbele kuwezesha vikundi vidogo vya wajasiriamali na wanalenga kuinua zaidi vikundi hivyo kwa kutoa mikopo yenye riba nafuu.

Mbali na utoaji mikopo, benki hiyo pia imepanga kwenda maeneo ya vijijini ili kuwa karibu zaidi na wakulima wadogo na kuwajengea uwezo wa kufanya kilimo cha kisasa zaidi.

“Kwa miaka hii mitano ambayo tumetoa huduma katika benki yetu, tunajivunia kwamba kwa kiasi fulani kutoa huduma bora kwa watanzania, ambalo ndilo lengu kuu la benki yetu, lakini pamoja na mambo mengine tumetoa huduma hiyo kwa wajasiriamali wadogo. Na katika awamu hii ya serikali ambayo imejizatiti kujenga Tanzania ya viwanda, na sisi tumeona tuiunge mkono kwa kupeleka huduma hii vijijini kwa wakulima, kwa sababu tunaamini kwamba endapo tutawawezesha kwa kuwapa elimu namna ya kujikita katika kilimo cha kisasa na tukawapatia pia mikopo ya riba nafuu”. Amefafanua Mwangalaba

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter