Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Mengi atoa neno kwa wajasiriamali

Mengi atoa neno kwa wajasiriamali

0 comment 111 views

Mwenyekiti wa kampuni ya IPP Media na mjasiriamali Dk. Reginald Mengi ametoa wito kwa watanzania kutokata tamaa na kujiamini hususani wanapoamua kufanya shughuli za ujasiriamali. Dk. Mengi amesema hayo alipokutana na wajasiriamali wa asasi ya Entrepreneur Organization (EO) tawi la Tanzania, ili kuwapa historia na uzoefu wake katika ujasiriamali hasa kuhusu kitabu chake alichozindua hivi karibuni.

Mengi amewataka watanzania kuchukua hatua za makusudi sambamba na kuongeza jitihada zaidi katika kuzikimbilia fursa za kiuchumi kwa kuongeza uzalishaji ili kuendana na wakati huu ambao serikali ya awamu ya tano imekuwa ikihamasisha kuhusu viwanda na uwekezaji  huku akisisitiza uthubutu na kujiamini kama njia mojawapo ya kutekeleza mipango kwa vitendo.

Akitolea ufafanuzi juu ya kusudio kubwa la kitabu cha “I Must, I Can, I Will,” Mengi amesema alishauriwa na mwanae kuandika kitabu hicho ili kuwahamasisha watanzania kuwa na uthubutu pamoja na kuwapa elimu juu ya kuzitumia fursa za kiuchumi zinazowazunguka. Mengi amewataka watanzania kujifunza na kuwa wabunifu katika masuala mbalimbali yanayohusu ujasiriamali ikiwemo kutunga sera zenye kuhamasisha uzalishaji ili kuipeleka Tanzania katika uchumi wa kati.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter