Home KILIMO Wakulima washauriwa kupima udongo

Wakulima washauriwa kupima udongo

0 comment 105 views

Mratibu wa Wabia kutoka Kituo cha kuendeleza kilimo nyanda za juu kusini mwa Tanzania (SAGCOT) Adam Ndaturu ametoa wito kwa wakulima kuwa na utaratibu wa kupima udongo wa mashamba yao kabla ya msimu kuanza ili wafahamu upungufu uliopo na kupatiwa ushauri wa mbolea na mazao wanayoweza kutumia ili kufanya kilimo chenye tija na kuongeza uzalishaji.

Ndaturu amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha zoezi la kutoa elimu kwa vitendo kwa wakulima mkoani Njombe ambapo amesisitiza kuwa ni muhimu kupima udongo kabla ya kutumia mbolea ili kufahamu kiasi halisi cha mbolea kinachotakiwa.

“Wakulima wengi hawana tabia ya kupima udongo ili kujua tatizo lililopo kabla ya kutumia mbolea na wengi wamekuwa wakitumia mbolea kwa mazoea bila kujua tatizo la udongo”. Amefafanua Mratibu huyo.

Pamoja na hayo, Ndaturu amedai kuwa SAGCOT inaendelea kufanya kazi kubwa ili kuhakikisha pembejeo zinapatikana kwa wakati an kuongeza kuwa wanaendelea kutoa elimu katika maeneo mengine ya mkoa huo ili kuwafikia wakulima wengi zaidi lengo kuu likiwa ni kuchochea kilimo chenye tija ili taifa lijitosheleze kwa chakula.

“Tayari wataalamu wa kupima udongo wapo mkoani Njombe hivyo ni wakulima kuhimizaba kuwatumia wataalamu hawa wakapima maeneo yao na kupatiwa ushauri. Gharama za kupima shamba ni Sh. 30,000 kwa mkulima mmoja na hupungua zaidi kwa wakulima watakaojiunga katika vikundi”. Ameeleza Mratibu huyo.

 

.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter