Home VIWANDAMIUNDOMBINU Mbarawa ataka vyanzo vya maji kutunzwa

Mbarawa ataka vyanzo vya maji kutunzwa

0 comment 95 views

Waziri wa Maji, Prof. Makame Mbarawa amezindua kampeni ya kupanda miti kandokando ya vyanzo vya maji nchi nzima mkoani Mtwara ili kuhakikisha vyanzo hivyo vinatunzwa na kuwa endelevu kwa miaka ijayo. Waziri Mbarawa amezindua kampeni hiyo katika halmashauri ya wilaya ya Mtwara mjini na kuagiza bodi zote za mabonde tisa nchini kuwa na mipango madhubuti ya kusimamia na kutunza rasilimali za maji kutokana na uharibifu mkubwa unaoendelea, hali inayohatarisha maji kupungua kufuatia vyanzo vingi kukauka, hali inayoweza kusababisha ukosefu wa maji ya kutosha kwa ajili ya miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.

Katika maelezo yake, Prof. Mbarawa amesema Sheria ya Maji Namba 11 ya Mwaka 2009 hairuhusu mtu kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji, huku ikisistiza kuwa, shughuli zote zifanyike umbali wa mita 6o kutoka chanzo cha maji na kutaka maeneo yote kuwekwa mipaka na vizuizi kuonyesha ukomo wa watu kuingia kwenye vyanzo hivyo.

‘‘Hatutaki kupata hasara kwenye miradi tunayowekeza fedha nyingi, halafu baadae iwe kama magofu kwa kukosa maji. Imefika hatua kuwa ni lazima tuchukue hatua za lazima kuinusuru taifa letu na uhaba wa maji. Niwatake wananchi watoe ushirikiano wa karibu na serikali kuhakikisha vyanzo vyetu vyote vinakuwa endelevu kwa kuzalisha maji ya kutosha na kuwa na uwezo wa kutoa huduma ya uhakika kwa miaka ijayo. Kwa kuanza tumepanda miti nane katika chanzo hiki cha Mtawanya, nataka ifikapo Desemba mwaku huu, nikute zaidi ya miti 1,000 kwenye chanzo hiki na zoezi hili lifanyike nchi nzima kwa sababu kama Waziri mwenye dhamana ya kusimamia rasilimali za maji, nitalisimamia jambo hili ipasavyo’’. Amesema Waziri Mbarawa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter