Home AJIRA Vijana washauriwa kuacha kuchagua kazi

Vijana washauriwa kuacha kuchagua kazi

0 comment 92 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ametoa wito kwa vijana hapa nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi na kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi mikubwa iliyo chini ya serikali ikiwemo ya ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme, barabara, upanuzi wa bandari na ujenzi wa miundombinu ya nishati. Majaliwa ametoa ushauri huo wakati wa maadhimisho ya miaka 73 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) ambayo kwa mwaka huu yamebeba ujumbe unaosema, ‘Uwezeshaji wa vijana na ubunifu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu’

Waziri Majaliwa amefafanua kuwa serikali inatambua uwepo wa changamoto ya ajira na hiyo imepelekea kuanzishwa kwa mikakati mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo vijana. Waziri Mkuu ametaja mikakati hiyo ni pamoja na kuanzisha wakala wa ajira, mafunzo ya kazi kwa vijana na sera ya ajira. Mbali na hayo, Majaliwa amesema bado kuna changamoto ya ajira na kuomba UN kuwapa nafasi za ajira, mafunzo kwa vitendo na fursa za kujitolea zinapojitokeza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter