Home KILIMO Wakulima wapigwa ‘stop’ kuuza kahawa ghafi

Wakulima wapigwa ‘stop’ kuuza kahawa ghafi

0 comment 115 views

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kahawa Nchini (TACRI), Dk. Deusdedit Kilambo amesema kuanzia hivi sasa, kahawa wakulima hawatoruhusiwa kuuza kahawa zenye maganda (kahawa ghafi) kutokana na kwamba kufanya hivyo kunashusha thamani na ubora wa zao hilo, hali inayopelekea kahawa ya hapa nchini kushuka thamani katika soko la dunia. Dk. Kilambo amesema hayo wakati akizungumza katika ziara ya maofisa wa kijeshi kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliopo kwa jili ya mafunzo katika Chuo cha kijeshi cha Duluti mkoani Arusha.

“Kukosekana kwa bei katika soko la dunia kwa kahawa yetu kunatokana na wakulima sisi wenyewe. Tupo katika harakati za kuiongeza thamani kahawa yetu…itakuwa ni jambo la aibu kama serikali ikiendelea kuwaacha watu kuuza zao hilo bila kukobolewa kitaalamu kwa kufanya hivyo ni kuipunguza thamani na ubora na bei kushuka”. Ameeleza Dk. Kilambo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unidhamu cha Duluti, Brigedia Jenerali Ibrahimu Mhona amesema wanalenga kujifunza kwa vitendo yale waliyosoma darasani hususani teknolojia katika kukuza uchumi wa kati na wa viwanda na kuongeza kuwa wapo tayari kutekeleza sera ya kukuza uchumi na viwanda kwa vitendo utakaosaidia watanzania wengi kuajiriwa na kujiajiri ili kutokomeza changamoto ya ajira.

“Tumefika kwenye taasisi hii tumejionea mengi..tumejifunza mengi..lakini kubwa tumeelezwa jinsi ambavyo zao la kahawa linavyoweza kukuza pato la taifa pamoja na njia gani bora za kulima ili kufikia azma hiyo..tumepokea na tutakuwa waelimishaji kwa vitendo”. Amesema Brigedia huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter