Home BIASHARA Waziri Tizeba atoa neno TRA

Waziri Tizeba atoa neno TRA

0 comment 90 views

Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia uwezekano wa kubadilisha mfumo wanaoutumia katika kukusanya kodi hivi sasa kwani mfumo huo sio rafiki kwa wafanyabiashara. Dk. Tizeba amesema hayo baada ya kutembelea banda la TRA katika maonyesho ya SIDO kitaifa yanayofanyika mkoani Simiyu. Waziri huyo amedai kuwa mfumo ambao TRA umekuwa sio rafiki kwa wafanyabiashara na kupelekea baadhi yao kushindwa kuendeleza biashara zao.

Dk. Tizeba amefafanua kuwa moja ya mfumo huo ni ule ambao mfanyabiashara anapaswa kulipa kodi ndani ya siku 90 kutoka siku ya kwanza aliyoanza kufanya biashara yake, hali ambayo amedai si haki kwa wafanyabiashara.

“Kwanini huyu mfanyabiashara anapoanza biashara yake asiachwe kwanza mpaka mwaka mzima ndipo aweze kulipa hiyo kodi, maana akifanya biashara mwaka mzima atakuwa tayari amepata faida na atalipa kodi, hawezi kukimbia maana amepata faida. Lakini kwa mfumo huu, miezi mitatu anatakiwa kulipa kodi haujui kama amepata faida au hajapata, mimi siukubali hata kidogo, hauko rafiki sana na wakulima wetu na wafanyabiashara, unawafanya kuacha na kukimbia bishara zao”. Amedai Dk. Tizeba.

Akiongelea maonyesho hayo kwa ujumla, Waziri Tizeba amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kuhakikisha wanajifunza teknolojia mbalimbali za ujasiriamali ili kuongeza uzalishaji kwenye bidhaa zao.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter