Home VIWANDAUZALISHAJI Utoroshwaji madini kudhibitiwa

Utoroshwaji madini kudhibitiwa

0 comment 67 views

Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema serikali inaendelea kujipanda na kuweka mikakati ili kudhibiti utoroshwaji wa madini katika maeneo ya uzalishaji na yale ya mipakani. Kairuki amesema hayo wakati akifungua jukwaa la sekta ya uzinduaji Tanzania ambapo ameeleza kuwa Wizara ya Madini imeweka vipaumbele ambavyo vitasaidia sekta hiyo kuimarika na kuwanufaisha watanzania wote. Waziri Kairuki ametaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na uwajibikaji katika sekta hiyo na uzinduaji kwa ujumla ikiwa ni pamoja na uimarishwaji wa ukusanyaji mapato ya serikali yanayotokana na rasilimali za madini.

“Tuna uhakika wa kufanikisha lengo hili kwa kuwa tuna mikakati madhubuti ya kuimarisha ukaguzi wa migodi mikubwa, ya kati na ya uchimbaji mdogo ili kupata taarifa sahihi za maeneo ya uwekezaji, uzalishaji, mauzo na kodi mbalimbali”. Ameeleza Waziri Kairuki.

Aidha, Waziri huyo amesema kuwa wataendelea kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na wale wa kati katika kuhakikisha wanatoka hatua waliyopo hivi sasa na hatimaye kuwa wachimbaji wakubwa.

“Wizara imetenga maeneo manne nchini kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kuendelea kutenga mengine na kwamba kabla ya kuyagawa yatabainishwa uwepo wa mashapo ya madini na taasisi yetu ya GST ya utafiti wa madini, ili kuepusha kufanya uchambuzi kwa kubahatisha”. Amesema Kairuki.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter