Home VIWANDAUZALISHAJI Dk. Tizeba apongeza uzalishaji pamba

Dk. Tizeba apongeza uzalishaji pamba

0 comment 103 views

Waziri wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba ametoa pongezi kwa wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wote wa mikoa inayozalisha pamba nchini kwa usimamizi bora uliopelekea uzalishaji wa zao hilo kuongezeka katika msimu wa mwaka 2018/2019. Dk. Tizeba ametoa pongezi hizo leo wakati akifungua mkutano wa 14 wa wadau wa sekta ndogo ya pamba jijini Mwanza na kuongeza kuwa, uzalishaji wa zao hilo katika msimu wa ununuzi wa mwaka 2018/19 umeongezeka kwa asilimia 67 na kufikia tani 221,600.

 

Mbali na hayo, Waziri Tizeba ametoa wito kwa viongozi hao kuongeza ufanisi wa usimamizi wa Pamba kwani pamoja na kuongezeka kwa uzalishaji, bado matarajio ya uzalishaji hayakufikiwa kwa mujibu wa makubaliano huku akitaja baadhi ya sababu zilizopelekea kupungua kwa uzalishaji kuwa ni pamoja na ukame, mlipuko wa wadudu wakiwemo viwavi jeshi vamizi, mvua kubwa kati ya Machi na Mei iliyopelekea kuzama kwa pamba kwenye maeneo yote ya mbuga na mabondeni pamoja na ufahamu mdogo wa wakulima.

 

Aidha, Dk. Tizeba ameitaka Bodi ya Pamba kugawa kamba za kupandia kabla ya tarehe 10 Novemba 2018. Waziri huyo pia amezungumzia uamuzi wa serikali kubadilisha mfumo wa kununua pamba ulipokelewa kwa hisia mbalimbali lakini vyama vya ushirika vya msingi vimesimamia kwa ufanisi mkubwa zoezi hilo.

 

“Natambua yapo mapungufu yaliyojitokeza katika shughuli ya ununuzi wa pamba ikiwemo AMCOS kupoteza fedha za makampuni ya pamba mfano wilaya ya Maswa na kuchelewesha kulipa baadhi ya wakulima katika Wilaya za Bunda na Serengeti”. Amesema Waziri Tizeba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter