Home VIWANDANISHATI Vijiji 25 kuunganishwa gridi ya taifa

Vijiji 25 kuunganishwa gridi ya taifa

0 comment 102 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amesema takribani vijiji 25 kati ya vijiji 55 mkoani Njombe vimeunganishwa katika mradi wa umeme wa kilovoti 220 mradi wa Makambako–Songea, mradi ambao umeigharimu Sh. 216 bilioni na kufanya wilaya ya Ludewa kuunganishwa katika gridi ya taifa tangu kuanzishwa kwa wilaya hiyo mwaka 1975. Dk. Kalemani amesema hayo wilayani Ludewa aliposhiriki kuzima mtambo wa umeme unaotumia mafuta mazito na kuwasha ule unaotumia gridi ya taifa uliounganishwa kutoka kituo cha Madaba.

 “Kituo hiki kilikuwa na mashine ya kutumia mafuta mazito yenye uwezo mdogo ilikuwa na uwezo wa megawati 0.5, kwa mtambo huu peke yake tulikuwa tunatumia zaidi ya Sh. 75 milioni kwa kuwasha na kuzima kwa mwezi katika wilaya ya Ludewa”. Ameeleza Waziri Kalemani.

Katika maelezo yake, Waziri huyo amesema kuwashwa kwa mitambo hiyo kutaiwezesha serikali kuokoa takribani Sh. 9 bilioni kutokana na kuzimwa kwa umeme wa mafuta mazito baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa ya umeme wa maji kupitia kituo cha kusambazia umeme cha Makambako–Songea. Waziri Kalemani amesisitiza kuwa vijiji vyote vya wilaya hiyo vitapatiwa huduma ya umeme hadi kufikia mwezi Aprili mwaka 2019.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter