Home BENKI BoT yaongeza muda usimamizi wa Bank M

BoT yaongeza muda usimamizi wa Bank M

0 comment 132 views

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetangaza kuongeza muda wa siku sitini (60) zaidi wa usimamizi wa Bank M Tanzania Plc (Bank M) kuanzia tarehe 2 Novemba 2018. BoT ilichukua usimamizi wa benki hiyo tangu 02 Agosti 2018 baada ya kugundulika kuwa benki hiyo ilikuwa na upungufu mkubwa wa ukwasi kinyume na mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya Mwaka 2006 na taratibu zake. Baada ya kuchukua usimamizi, Benki Kuu ilisitisha utoaji wa huduma za kibenki za Bank M kwa takribani siku tisini (90) ili kutathmini hatua za kuchukua na kupata suluhisho la suala hilo.

 

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuarifu umma kuwa mchakato wa kutathmini hatua za kuchukua ili kupata ufumbuzi wa matatizo ya Bank M haujakamilika; hivyo muda wa usimamizi umeongezwa kwa kipindi cha siku 60 kuanzia tarehe 2 Novemba 2018”. Imesoma taarifa iliyotolewa kwa umma.

 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kuweka mbela na kulinda maslahi ya wananchi wote wenye amana katika mabenki ili lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter