Home VIWANDANISHATI Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini yavunjwa

Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini yavunjwa

0 comment 133 views

Kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa, amevunja bodi hiyo iliyoundwa mwaka jana kwa mujibu wa Sheria ya Wakala Vijijini No. 8 ya mwaka 2005.

“Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu 9 (3) (b) cha Sheria No. 8 ya Nishati Vijijini ya 2005, nimeamua kuivunja Bodi kwa kutengua uteuzi wa mwenyekiti pamoja na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini kuanzia leo” Amesema Dk. Kalemani.

Bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Gideon Kaunda imedumu kwa kipindi cha mwaka mmoja pekee. Wajumbe waliotenguliwa nafasi zao katika Bodi hiyo ni pamoja na Happiness Mhina, Stella Mandago, Scholastica Jullu, Mhandisi Innocent Lwogwa, Amina Chinja,Teobard Sabi na Michael Nyagoga.

Aidha Waziri Kalemani ameeleza kuwa bodi nyingine itaundwa baadae kwa mujibu wa Sheria ya Nishati Vijijini ya Mwaka 2005.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter