Home FEDHAHISA Wanahisa Vodacom wakubali hisa za Rostam Aziz kuuzwa

Wanahisa Vodacom wakubali hisa za Rostam Aziz kuuzwa

0 comment 199 views

Baada ya kufanya mkutano mkuu wa dharura, wanahisa wa kampuni ya Vodacom wameikubalia kampuni ya Vodacom Group kununua asilimia 25.25 ya hisa ambazo hapo awali zilikuwa zikimilikiwa na kampuni ya Mirambo Holdings iliyo chini ya mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz. Mkutano huo umefanyika jijini Dar es salaam ambapo kwa mujibu wa Mkaguzi wa ndani wa hesabu za fedha Alvin Kajula, asilimia 88.18 ya wanahisa wa kampuni hiyo wameridhia mauzo hayo yatakayoifanya kampuni ya Vodacom Group kuwa na umiliki mkubwa zaidi.

Hii inakuwa mara ya pili kwa Aziz kuuza hisa anazomiliki katika kampuni hiyo tangu mwaka 2014 ambapo aliuza asilimia 17.2 ya hisa zake kwa Dola za Marekani 240 milioni. Vodacom Tanzania ni ya pili kwa kuchangia faida na mapato ya Vodacom Group kwa kuwa na jumla ya wateja waliosajiliwa milioni 13, ikiwa chini ya Afrika Kusini ambapo mtandao huo una watumiaji zaidi ya milioni 23.

Mpango wa Vodacom Group kununua hisa za Vodacom Tanzania uliwekwa wazi tangu Februari mwaka jana na hadi sasa, taratibu zimeshakamilika. Tume ya Ushindani wa Biashara Tanzania (FCC) ilitoa tangazo la mpango wa Vodacom Group kununua hisa za Vodacom Tanzania mwezi Mei na kuruhusu yoyote mwenye pingamizi na mpango huo kuwasilisha hoja zake.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter