Home FEDHAMIKOPO Wakulima itumieni TADB-Majaliwa

Wakulima itumieni TADB-Majaliwa

0 comment 58 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wakulima mkoani Tabora kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili wapate nafasi ya kuongeza uzalishaji katika shughuli zao. Majaliwa amesema hayo alipokuwa akizungumza kwenye jukwaa la uwezeshaji mkoani humo na kueleza kuwa nia kuu ya serikali kuanzisha benki ya kilimo ni kuwakomboa wakulima na kuwawezesha kufanya kilimo biashara.

“Napenda kuwashauri wawekezaji binafsi na taasisi mbalimbali mkoani Tabora tumieni fursa za mabenki ikiwemo Benki yenu ya kilimo kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo na mifugo. TADB inafanya vizuri sana hata Mheshimiwa Rais Magufuli ameisifu pia. Wakati ndio huu wa kujiimarisha katika kilimo. Tumieni uwepo wa Benki yenu ya kilimo kupata mikopo kupanua wigo wa shughuli zenu za kilimo na mifugo”. Amesisitiza Majaliwa.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amesema mkoa huo umejipanga kuhakikisha unaweka mazingira rafiki kwa ajili ya wawekezaji ikiwemo kuondoa urasimu katika usajili wa ardhi na kutoa vibali. Naye Meneja wa TADB katika ukanda huo. Geofrey Mtawa ameeleza kuwa benki hiyo inatoa mikopo inayolenga kutatua changamoto mbalimbali zilizopo katika mnyororo wa thamani.

“Tunatoa mikopo kwa ajili ya maghala ya kuhifadhia mazao, ununuzi wa zana bora za kilimo”. Amesema Mtawa.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter