Home BENKI NMB yatoa msaada wa mamilioni Arusha

NMB yatoa msaada wa mamilioni Arusha

0 comment 92 views

Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya shule venye thamani ya Sh. 20 milioni katika wilaya ya Arumeru mkoani Arusha ikiwa ni jitihada ya benki hiyo kuungana na serikali katika jitihada zake za kuimarisha sekta ya elimu hapa nchini. Alizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Kaimu Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini, Cosmas Gabrieli amesema benki hiyo inatambua juhudi za serikali kwa kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka kidato cha nne. Benki hiyo imetoa msaada wa meza 166 za maabara, mabati 166, madawati 62 pamoja na meza 62.

Wakizungumza mara baada ya Mkuu wa wilaya hiyo kupokea msaada huo, baadhi ya wakazi ambao walipata nafasi ya kuhudhuria hafla hiyo wamesema benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kuchochea maendeleo katika jamii hususani katika sekta ya elimu.

“Tunaishukuru benki ya NMB kwa msaada huu mkubwa kwa kuwa watoto wetu walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu na wakati mwingine wanafunzi wa kike walikuwa wanarubuniwa kwa kupewa lifti na madereva bodaboda, hali iliyokuwa inawasababishia kupata ujauzito na kuacha masomo”. Amesema mkazi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter