Home BIASHARA Vodacom Tanzania PLC yawatunuku watumiaji wa mtandao bomba Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1

Vodacom Tanzania PLC yawatunuku watumiaji wa mtandao bomba Pointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1

0 comment 131 views

Vodacom Tanzania PLC,kampuni ya simu nambari moja nchini, inagonga kengele za shangwe katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunukia wateja wake pointi za Tuzo zenye thamani ya Shilingi bilioni 1 kama sehemu ya mpango wa kampuni kuwashukuru wateja wao

Programu hii ni ya kwanza kabisa iliyoletwa na kumpuni hiyo ambayo inawapatia wateja wake pinti za tuzo kila waongezapo salio au kufanya miamala ya M-Pesa. Wateja wanaweza kutumia pointi hizo kwa kuzibadili kupitia waleti zao za M-Pesa, kununua bando, na pia kwa kununua bidhaa mbalimbali katika maduka ya Vodacom.

“Mapato ya Vodacom Tanzania yaliongezeka kwa asilimia 6 katika mwaka huu, na ukuaji huuumechangiwa sana na wateja wetu. Hivyo Pointi za Tuzo ni njia ya kuonyesha shukrani zetu kwa watumiaji wetu na kwa moyo wa kutoa, tumeamua kufanya jambo la ziada katika msimu huu wa sikukuu kwa kuwatunuku wateja wetuPointi za Tuzo zenye thamani ya shilingi bilioni 1,”alisemaHisham Hendi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji. “Ninawahimiza wateja wetu kuishi maisha ya ki-Tuzo, kununua muda wa maongezi na kufanya miamala mingi kadri inavyowezekana katika M-Pesa hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na kujipatiapointi hapo hapo kila wafanyapo miamala hiyo,” aliongeza Hisham.

Wateja hao wanatunukiwa Pointi za Tuzo 50 kwa kila Shilingi 500 wanayotumia kununua salio. Pointi hizi zaTuzo zinaweza kulimbikizwa hadi miezi 12 tangu mtu aanze kujikusanyia na baada ya miezi hiyo 12 zisipotumiwa muda wake huisha. Wateja wa Vodacom wanaweza pia “Kulipa kwa Pointi” moja kwa moja kwa wafanyabiashara wanaopokea M-Pesa, kwa kupiga *149*01#>TUZO>TUZO POINTS>Vuna Pointi> (Nunua bando/Lipa/Badili kwa M-Pesa).

“Mwaka mzima, wateja wetu wamekuwa ndiyo walengwa na kiini cha ubunifu wetu – Vodacom Tanzania tumedhamiri kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora kabisa,” alimalizia Hisham.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter