Home KILIMO UWWKT wampongeza Rais Magufuli

UWWKT wampongeza Rais Magufuli

0 comment 109 views

Mwenyekiti wa Umoja wa Wabanguaji Wadogo wa Korosho Tanzania (UWWKT), Tumpale Magehema amesema uamuzi wa Rais Magufuli kununua korosho za wakulima na kuzibangua hapa nchini umepongezwa na umoja huo. Magehema amesema hayo wakati akisoma risala mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya na kuongeza kuwa, uamuzi huo wa Rais unategemea kuwapatia ajira wanachama wake takribani 2,881, hivyo ni jambo la kupongezwa. Licha ya kutoa ajira, Mwenyekiti huyo amesema uamuzi huo utaongeza ari ya kufanya kazi na kuchochea ukuaji wa uchumi hasa katika mikoa inayolima korosho kwa wingi.

Katika taarifa yake, Katibu wa umoja huo, Audax Mkongi,amesema tangu kuanzishwa kwa umoja huo mwaka 2015, wamefanikiwa kumiliki mashine za kubangua korosho ghafi kwa kutumia mkono 117, mashine za kutumia miguu 317, mashine za kuchemshia (boiler) 23, mashine za kupanga madaraja 12, mashine za kukaushia 12, na za kufungashia 14 zilizo na uwezo wa kubangua korosho ghafi Kilo 25,370 kwa siku.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Stella Manyanya ametoa pongezi kwa umoja huo kwa jitihada wanazofanya kuunga mkono serikali ya awamu ya tano ya uchumi wa viwanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter