Home BIASHARAUWEKEZAJI Serikali yawekeza mabilioni kupeleka mawasiliano vijijini

Serikali yawekeza mabilioni kupeleka mawasiliano vijijini

0 comment 106 views

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kila mwananchi anapaswa kuwa na mawasiliano ya uhakika kwani dunia hivi sasa ipo kiganjani. Waziri Kamwelwe amesema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini baina ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kampuni nne za simu za mkononi ambazo zilizopatiwa ruzuku na Sh. 173 bilioni na serikali kwa ajili ya kupeleka huduma za mawasiliano vijijini kwenye kata 173 zilizopo maeneo mbalimbali nchi nzima.

Kampuni zilizosaini mkataba wa kupeleka mawasiliano ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kampuni ya Vodacom Tanzania, Kampuni ya Viettel Tanzania (Halotel) na Kampuni ya MIC Tanzania (Tigo).

“Tumekubaliana na Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuwa waanze kutoa huduma za kifedha na watumie huduma za Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili mawasiliano yaweze kufika vijijini kwa kuwa TPC na TTCL ni taasisi kongwe na wana mtandao mpana wa ofisi zao nchi nzima”. Amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa UCSAF Mhandisi Peter Ulanga amesema kampuni hizo za mawasiliano zimeshinda zabuni ya awamu ya tatu ya kupeleka mawasiliano kwenye kata 178 kwa gharama ya Sh. 28 bilioni. Mhandisi Ulanga ameongeza kuwa, hadi sasa UCSAF imepeleka mawasiliano kwenye takribani kata 703 nchi nzima ili kuboresha maisha ya wananchi kupitia TEHAMA.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter