Home BENKI UBA yamchangia mama aliyejifungua mapacha walioungana bima ya afya na nyumba ya thamani ya TZS 16,080,000

UBA yamchangia mama aliyejifungua mapacha walioungana bima ya afya na nyumba ya thamani ya TZS 16,080,000

0 comment 56 views

Mfuko wa  Benki ya UBA  leo umechangia TZS 16,080,000 kwenye ujenzi wa vyumba viwili  pamoja na kutoa bima ya afya kwa mapacha waliotenganishwa baada ya kuungana.

Akiongea wakati wa makabidhiano, Usman Isiaka, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya UBA alisema, “ Tuliposoma kwa mara ya kwanza ripoti ya mama wa hawa mapacha,  Mama Esther Simon tuligundua hakua na bima ya afya ambayo ingewaisadia kupata huduma ya afya wakiugua.  Kutokana na hii benki ya UBA Tanzania ikafanya jitihada ya kuwapatia bima ya miaka 10”.

Utoaji wa kadi za bima kwa mapacha ulifanyika Jumatano tarehe 7, Novemba 2018 ikishuhudiwa na Prof. Martin Corbally kutoka Ireland ambaye anafanya shughuli zake Bahrain pamoja Mtaalam wa upasuaji wa watoto hospitali ya Muhimbili, Dr. Petronia Ngiloi, ambaye alifanya upasuaji huo kwa masaa matano.

“Mkurugenzi Mtendaji wa UBA aliendelea kusema,” Tulimtembelea Bi. Simon Muhimbili na kuambiwa hawezi kuruhusiwa  kutoka  kutokana na mazingira mobovu ya nyumbani ambayo yasingeweza kuhakikishia uhai wa mapacha. Tulitembelea nyumba ya Bi.simon  na kuguswa mpaka kufikia kuisadia familia kuwajengea nyumba mpya’’.

Kuongezea kwa mfuko wa UBA, wafanyakazi wa UBA Tanzania wamechangia TZS 2,000,000 kwenda kwenye ulezi wa mapacha na mama yao.

Akiongea pia kwenye tukio hilo, Emeke E. Iweriebor, Mkurugenzi wa UBA Afrika Mashariki na Kusini alisema, “Msaada kwa Bi.Simon na wanawe mapacha inasukumwa na imani kubwa ya mfuko wa UBA, ambao ni vitu vikubwa vinafanyika tukishirikiana pamoja.  Tutaendelea kujikita katika kugusa maisha ya watanzania kwa kushirikiana na jamii husika katika elimu na mipango kama hii.

Mapacha wa kiume waliozaliwa Julai 12th 2018 katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani waliungana kwenye maini. Mapacha hao walitenganishwa kwa upasuaji wa kihistoria uliofanyika hospital ya taifa ya Muhimbili. Upasuaji huu ni wa aina yake tangu wa kwanza kufanyika miaka 24 iliyopita.

“ Nashukuru mfuko wa UBA kwa kumsaidia Bi. Simon na familia yake, na kuongezea kwenye msaada uliotolewa na mfuko, wilaya itatoa eneo ambalo nyumba mpya kwa ajili ya mapacha itajengwa. Nawakaribisha pia watanzania kuisadia familia hii namna yeyote ile. Wataoguswa wanaweza pia kuchangia kwenye akaunti ya akiba ya UBA special U- care, akaunti namba 56010560001396 Gracious Michael Mkono na Precious Michael Mkono ambayo imefunguliwa mahususi kwa ajili ya mapacha”, alisema  Mkuu wa wilaya ya Kisarawe,Jokate Mwegelo.

“Napongeza juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kutengenza mazingira wazeshi katika hospitali ya Muhimbili ambayo yamewezesha kufanyika kwa upasuaji kwa mafanikio na kuendelea kusaidia afya ya mama na watoto wake hadi sasa. Natambua pia msaada wa Mheshimiwa Jokate Mwegelo, Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, ambaye ametoa msaada wa eneo la kujengwa nyumba ya mapacha”, alihitimisha Mkurungezi  Mtendaji wa UBA Tanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter