Home KILIMO Kahawa yawanoa maafisa ugani

Kahawa yawanoa maafisa ugani

0 comment 113 views

Maafisa ugani 30 mkoani Kilimanjaro wamepigwa msasa juu ya kilimo bora cha kahawa hasa kuzingatia kanuni za zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kukuza pato la wananchi na mkoa kwa jumla.

Mafunzo hayo yalitolewa na shirika la Cafe Africa ambalo limeamua kujikita katika zao hilo kwa kuwa ni moja ya mazao makubwa ya kibiashara yanayoingizi nchi fedha za kigeni huku likiwa ni zao pendwa na serikali kama vile korosho na pamba.

Dafrosa sanga ambaye ni meneja uzalishaji wa kampuni ya Cafe Africa amesema lengo la mafunzo hayo ni kutoa elimu kwa vitendo kuanzia kuotesha miti,kuitunza na kuvuna ili maafisa ugani hao waweze kuwasaidia wakulima kuboresha kilimo cha zao la kahawa.

Pia mkuu wa wilaya ya moshi mheshimiwa Kipi Warioba aliwaasa maafisa ugani hao kuacha kujifungia ofisini bali waende shambani kuhakikisha wakulima wanapata elimu ya uzalishaji bora ili kukuza uchumi wa mkoa huo ikizingatiwa bei ya kahawa katika soko la dunia ni nzuri ikilinganishwa na mazao mengine ya biashara.

Mafunzo hayo kwa maafisa hao ugani yalitolewa kwa ushirikiano wa jukwaa la wadau wa kahawa (ANSAF) na shirika la Cafe Africa lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa zao hilo ili kukuza uchumi wa mkoa na nchi kwa ujumla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter