Home BIASHARA Mwenyekiti Fastjet adai serikali imemzuia kuleta ndege nchini

Mwenyekiti Fastjet adai serikali imemzuia kuleta ndege nchini

0 comment 175 views

Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania, Lawrance Masha amesema amezuiwa na serikali kuingiza ndege za shirika hilo nchini humo. Masha amesema hayo wakati wa mazungumzo na gazeti la Mwananchi na kufafanua kuwa, anatarajia mambo yatakuwa mazuri baada ya kumalizika kwa sikukuu.

Katika maelezo yake Masha ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani amesema serikali haitoi ushirikiano wa kutosha katika jitihada zake za kulifufua upya Shirika la Fastjet na kudai amezuiliwa kuingiza ndege aina ya Boeing 737-500 baada ya ile iliyokuwepo kuzuiliwa kufanya safari na TCAA kwa madai ya kuwa na hitilafu mara kwa mara na vilevile kutokana na Shirika kukosa Meneja anayewajibika.

Mwenyekiti huyo amesema endapo atapata ruhusa, ndege hiyo itawasili nchini kutoka Afrika Kusini ndani ya muda mfupi kwani kila kitu kipo tayari. Katika maelezo yake Masha amesema ndege iliyozuiwa tayari ilikuwa imelipiwa ikiwa na wafanyakazi wote, hivyo kuizuia ni hasara.

“TCAA inasema ili niweze kuingiza ndege hiyo nimalize kwanza madeni yote, baadhi ya madeni tayari yamelipwa na Fastjet Plc mengine Fastjet Tanzania. Tayari tumemaliza lakini fedha imeisha, kwa kuwa tayari fedha nyingine tulizitumia kutimiza matakwa yao, wangeniruhusu nifanye kazi ili nipate fedha ya kulipa yaliyobaki”. Ameeleza Masha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter