Vicheko,nderemo na vifijo vimetawala vinywani mwa wakulima waliopo halmashauri ya songea mkoani Ruvuma baada ya Waziri Mkuu wa Tanzania,Kassim Majaliwa kufungua mradi wa kuhifadhia nafaka pamoja na soko la mazao la OTC-lilambo.
Soko hilo lililofunguliwa January 3 ambayo ni siku ya pili kati ya nne za ziara ya waziri mkuu mkoani humo yenye lengo la kukagua shughuli za maendeleo limegharimu kiasi cha shilingi 1.5 bilioni ambapo pia maghala mawili yenye uwezo wa kuhifadhi tani 5000 za nafaka yalizinduliwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya waziri mkuu kwa vyombo vya habari imeelezea waziri ameridhishwa na viwango vya ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala huku akifafanua kuwa licha ya kuuza na kuhifadhi mazao pia wakulima watapata mafunzo namna ya kudhibiti wadudu na kuhifadhi mazao yao pamoja na taarifa za soko.
Mbali na wakulima pia majaliwa aliwaagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha wanalitangaza katika vyombo vya habari ili wakulima wawe wanapeleka mazao yao sokoni hapo.
Waziri mkuu amekua katika ziara ya mbalimbali ndani ya nchi zenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo ambapo katika ziara hiyo aliambatana na waziri wa kilimo Japhet Hasunga na Waziri wan chi,Ofisi ya waziri mkuu sera,bunge,kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu Jenista Mhagama,mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme na Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk Damas Ndumbaro.