Home KILIMO Mikataba ubanguaji korosho kusainiwa Januari 10

Mikataba ubanguaji korosho kusainiwa Januari 10

0 comment 104 views

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amesema Januari 10 mwaka huu, serikali itasaini mikataba na wamiliki wa viwanda vya ubanguaji wa korosho waliojitokeza kubangua korosho za serikali za msimu wa mwaka 2018/2019. Waziri Hasunga amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara na kueleza kuwa, hivi karibuni serikali ilitangaza kuwa korosho ghafi zote zitabanguliwa nchini hivyo utekelezaji wa zoezi hilo umeanza na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko itaingia mikataba ya ubanguaji.

“Wananchi wenye uwezo wa kubangua tunawaomba waende Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo-SIDO) kwa ajili ya kujiandikisha ambapo mpaka sasa watu 126 kwa ajili ya ubanguaji na tani 29 zimechukuliwa kwa ajili ya kuanza kubanguliwa”. Amesema Waziri Hasunga.

Pamoja na hayo, Waziri huyo amempongeza Rais Magufuli kwa kushuhudia utiaji saini mkataba wa mauziano ya mahindi baina ya Wakala wa Taifa wa hifadhi ya Chakula (NFRA) na Shirika la Chakula Duniani (WFP) wa Bilioni 21 zitakazoiwezesha NFRA kununua mahindi kwa wakulima hivyo kuimarisha soko la nafaka nchini.

Kuhusu malipo ya korosho na uhakiki wa wakulima, Waziri Hasunga amesema kiasi cha korosho iliyokusanywa kwenye maghala makuu ni tani 203,938.3 wakati korosho iliyopo kwenye vyama vikuu vya ushirika ni tani 29,803.53 inayofanya jumla ya korosho yote iliyopokelewa kwenye vyama vya ushirika na maghala makuu kuwa tani 233,741.83, sawa na asilimia 84.7 ya lengo lililowekwa la ukusanyaji katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma na Pwani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter