Home KILIMOKILIMO BIASHARA Tanzania kuuza korosho Algeria

Tanzania kuuza korosho Algeria

0 comment 97 views

Baada ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dk. Damas Ndumbaro kukutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Algeria, Saad Belabed, serikali imetangaza masoko kwa ajili ya zao la korosho nchini Algeria. Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam, Dk. Ndumbaro amesema Algeria ipo tayari kununua korosho zote za Tanzania.

Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa mazungumzo hayo ni jitihada mojawapo ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli kuwakomboa watanzania kiuchumi kwa kutafuta masoko ya mazao ya wakulima nje ya nchi.

Mwaka jana, serikali iliingilia kati taratibu za mauzo ya zao la korosho kufuatia mgogoro wa bei kati ya wakulima na wafanyabiashara, ambapo wafanyabiashara walitangaza kununua korosho kwa Sh. 1,500 kwa kilo, bei ambayo ilipingwa vikali na wakulima hali iliyopelekea Rais Magufuli kutangaza uamuzi wa serikali kununua korosho zote za wakulima kwa sh 3,300 kwa kilo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter