Home KILIMO Mikataba ubanguaji korosho yasainiwa

Mikataba ubanguaji korosho yasainiwa

0 comment 164 views

Kwa niaba ya serikali, Mkurugenzi wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Tanzania Dk. Hussein Mansoor, ametia saini mikataba ya ubanguaji korosho ya awali na kampuni nne ambazo ni kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd, Micronix Mtwara, Korosho Afrika, na Micronix-Newala.

Kampuni hizo zimeingia mikataba ya tani 7,500 ambapo kampuni ya Hawte Investment Co. Ltd yenye uwezo wa kubangua tani 2,000 kwa mwaka ikiwa imesaini mkataba wa tani 1,500. Micronix Mtwara yenye uwezo wa kubangua tani 2,400 kwa mwaka imeingia mkataba wa tani 1,200. Kampuni ya Korosho Afrika ya Ruvuma yenye uwezo wa kubangua tani 5,000 kwa mwaka imeingia mkataba wa kubangua tani 2,400 huku Micronix Newala yenye uwezo wa kubangua tani 5,000 kwa mwaka ikiingia mkataba wa kubangua tani 2,400.

Akizungumza wakati wa utiaji saini, Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amesema serikali imepitia kwa umakini vifungu vyote vya kisheria kabla ya kuingia makubaliano na kampuni hizo huku akiongeza kuwa, zoezi la ubanguaji tayari lilikuwa limeanza kupitia Shirika la SIDO ambalo hadi sasa tayari limeajiri wafanyakazi 160.

Waziri huyo amesema serikali ina matumaini makubwa kuwa mikataba iliyosainiwa itazingatiwa kwa kufuata taratibu na masharti yote yaliyopo kwa mujibu wa Sheria.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter