Home BIASHARAUWEKEZAJI Zanzibar kujenga bandari ya mafuta, gesi asilia

Zanzibar kujenga bandari ya mafuta, gesi asilia

0 comment 65 views

Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein amesema serikali imeamua kujenga bandari ya mafuta na gesi asilia katika eneo la Mangapwani Unguja na hadi sasa, eneo la bandari hiyo tayari limepimwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara, matangi ya mafuta na umeme. Katika maelezo yake, Rais huyo amesema kuwa upembuzi yakinifu kwa hatua ya mwanzo umekamilika na eneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za wananchi waliokuwa na makazi eneo la mradi limetengwa.

“Baada ya majadiliano yaliyoanza mwaka 2013 baina ya serikali ya mapinduzi na serikali ya Ras Al Khaimah, hatimaye maafikiano yamepatikana”. Amesema Dk. Shein.

Rais huyo ameeleza kuwa kampuni ya maendeleo ya mafuta na gesi asilia ya Zanzibar (ZPDC) na kampuni ya RAK Gas ya Ras Al Khaimah zimetia saini mkataba wa uzalishaji wa mgawanyo wa mafuta na gesi asilia huku akiongeza kuwa, hivi sasa makampuni hayo yanafanya utafiti wa mafuta na gesi asilia katika maeneo yenye maji kidogo kisiwani Pemba na baada ya hapo, watafanya hivyo Unguja.

“Napenda niwaombe wananchi nyote muendelee kuwa na ustahimilivu na msubiri maelezo ya serikali kuhusu taarifa za mafuta na gesi asilia”. Amesema Rais Shein.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter