Home BIASHARAUWEKEZAJI Mashamba sita ya Mohamed Enterprises yarudishwa serikalini

Mashamba sita ya Mohamed Enterprises yarudishwa serikalini

0 comment 64 views

Kufuatia mapendekezo yaliyotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Korogwe, Serikali imefuta mashamba sita ya kampuni ya Mohamed Enterprises kutokana na kutoendelezwa kwa kipindi kirefu. Mashamba hayo yaliopo eneo la Mombo, Mabogo pamoja na Kwalukonge wilayani Korogwe yana ukubwa wa hekari 12,915.126 na kati ya mashamba 14 yanayomilikiwa na kampuni ya Mohamed Enterprises Mazinde wilayani humo.

Akizungumza mara baada ya kutembelea mashamba hayo, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Angeline Mabula amesema lengo ya serikali kufanya hivyo ni kujenga nidhamu kwa waliopewa rasilimali za serikali kuzingatia masharti pamoja na taratibu ya uwekezaji.

Dk. Mabula amefafanua kuwa mara baada ya Halmashauri ya wilaya ya Korogwe kupeleka mapendekezo ya kufutwa  kwa mashamba hayo, Wizara ya Ardhi ilifuatilia kuhusu madai ya kutoendelezwa kwa  mashamba ya kampuni hiyo na baada ya kujiridhisha ikawasilisha maombi hayo  kwa  Rais na kuridhiwa.

Pamoja na hayo, Naibu Waziri huyo amempongeza Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela kwa kusimamia maagizo mbalimbali tangu Rais Magufuli alipoanza kubatilisha mashamba ambayo hayajaendelezwa katika mkoa huo. Kwa upande wake, Shigela amewataka wananchi wa Korogwe kutovamia maeneo ya mashamba hayo hadi Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe itakapopanga matumizi bora ya ardhi hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter