Home BIASHARAUWEKEZAJI TANESCO yakaribisha wawekezaji Arusha

TANESCO yakaribisha wawekezaji Arusha

0 comment 140 views

Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) jijini Arusha Mhandisi Herini Mhina ametoa wito kwa wawekezaji kuwekeza katika viwanda mkoani humo kwani umeme upo wa kutosha. Mhandisi Mhina amesema kufuatia uwekezaji uliofanywa na serikali kwenye miradi mbalimbali ya umeme, uzalishaji umeongezeka na kuwezesha shirika hilo kutoa huduma za uhakika kwa wateja wakubwa, wadogo pamoja na wa kati.

“TANESCO Arusha tunakaribisha wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza kwenye sekta mbalimbali, tuna umeme wa kutosha, tunaamini viwanda ni njia ya kutupeleka katika uchumi wa kati. Kwa sasa mkoa huu unazalisha umeme wa megawati 120 ingawa mahitaji kwa sasa ni megawati 75 jambo linalifanya TANESCO kuwa na ziada ya umeme wa megawati 50. Uwekezaji uliofanywa na serikali katika sekta hii, umemaliza tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kama ilivyokuwa miaka ya nyuma”. Amesema Meneja huyo.

Aidha,Mhandisi huyo amesema uwekezaji uliofanywa na serikali kuboresha nishati ya umeme mkoani humo utazalisha matokeo mazuri kuelekea uchumi wa kati ikizingatiwa kuwa, jiji la Arusha ni kivutio kikubwa cha utalii.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter