Home VIWANDAUZALISHAJI Mchele wa Tanzania hatari

Mchele wa Tanzania hatari

0 comment 165 views

Mtaalamu wa Kilimo kutoka Jimbo la Zambezia nchini Msumbiji, Jaime Gado amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinazalisha mchele wenye ubora katika nchi za Msumbiji, Rwanda, Burundi na Kenya. Gado ameeleza hayo alipotembelea nchini akiwa na wataalamu wa zao hilo ili kubadilishana ujuzi na uzoefu na wakulima wa Tanzania kuhusu uzalishaji bora wa zao hilo.

“Tumeona changamoto kadha wa kadha, lakini bado mkulima huyu amekuwa akizalisha kilicho bora, tatizo ni uhakika wa soko, naishauri mamlaka husika kuangalia namna ya kuwasaidia wakulima, ili waweze kuuza kwa wingi katika nchi zinazozunguka bara la Afrika. Nipende pia kuwapongeza JICA kwa kuweka utaratibu wa kuongeza thamani ya zao hili, kwa kuwasaidia kusimamia makubaliano kati ya wanunuzi na wakulima kwa wakulima wa Tanzania kupitia kwenye mradi wa TANRICE, kwa kuwa umekuwa mkombozi kwa wakulima wengi hususani waliopo kwenye skimu ya Lower Moshi”. Amesema Mtaalamu huyo.

Kwa upande wake, Mtaalamu kutoka Tanzania, Shedrack Msemo amesema  baadhi ya changamoto wanazokumbana nazo wakulima ni pamoja na miundombinu mibovu na kutokuwa na mashine bora za ukoboaji na uvunaji mpunga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter