Home KILIMO Wakulima wachekelea punguzo la tozo mchuzi wa zabibu

Wakulima wachekelea punguzo la tozo mchuzi wa zabibu

0 comment 139 views

Wakulima wa zabibu jijini Dodoma kupitia Chama cha Wakulima wa Zabibu na Masoko Mpunguzi (UWAZAMAM) wametoa pongezi kwa Rais Magufuli na serikali kwa kupunguza tozo ya ushuru katika mchuzi wa zabibu kutoka Sh. 3,315 hadi Sh. 450. Kufuatia punguzo hilo, chama hicho kimewataka wanunuzi kufikiria kuongeza bei yao ya manunuzi kutoka Sh. 1,540 hadi Sh. 2,000 kwa lita ili wakulima waweze kunufaika na biashara hiyo.

“Kwa kuwa viwanda vikubwa vinavyochukua mchuzi huu vitakuwa vimepunguziwa kodi, basi tunaomba waangalie  uwezekano wa kuongeza bei kwenye ununuzi kutoka Sh. 1,540 hadi Sh. 2,000”. Amesema Katibu wa UWAZAMAM, Emmanuel Temba.

Katibu huyo amesema wamekuwa wakisindika mchuzi huo kutokana na hasara waliyokuwa wakiipata wakulima sababu ya kuharibika kwa zababu. Temba ameongeza kuwa, hadi sasa mchuzi huo umewaletea faida hivyo wanahamasika kutengeneza lita nyingi zaidi.

Ameitoa mifano ya faida zilizotokana na mauzo ya mchuzi huo kuwa, katika kipindi cha masika walinunua zabibu tani 19 zenye thamani ya Milioni 11.4 na kupata mchuzi lita 15,000 uliouzwa kwa thamani ya Shilingi 18 milioni Kwa mwaka 2016, walinunua tani 62.6 kwa Shilingi 75.1 Milioni na kupata mchuzi lita 48,000 uliouzwa kwa Shilingi 86.4 Milioni. Msimu wa kiangazi mwaka 2017 walinunua tani 108 kwa Milioni 129.6 na kupata mchuzi lita 84,000 uliouzwa Shilingi 151.2 milioni.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter