Home BENKI Benki zashauriwa kuchangamkia ubadilishaji fedha

Benki zashauriwa kuchangamkia ubadilishaji fedha

0 comment 102 views

Kufuatia sakata la kufungwa kwa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo, amezitaka benki kufikiria kutoa huduma kwa wananchi na watalii masaa 24. Wakati akifungua semina ya wafanyabiashara na wajasiliamali iliyoandaliwa na  benki ya CRDB, Gambo amesema  kufuatia kufungwa kwa maduka hayo, watalii mkoani humo wanapata changamoto kubwa ya kubadilisha fedha zao jambo ambalo linaweza kuhatarisha sekta ya utalii na uchumi. Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa mabenki mkoani humo  hasa CRDB kuchangamkia fursa hiyo kwa manufaa yao na ya uchumi wa nchi.

“Nakuomba Mkurugenzi ukipata fursa kakutane na Chama cha Mawakala wa Utalii (Tato) wakueleze changamoto zao na uone utasaidia vipi”. Amesema Gambo.

Hata hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, AbdulMajid Nsekela ameeleza kuwa, hadi sasa benki hiyo imetumia fursa hiyo kufungua dirisha maalum kwa ajili ya kubadilisha fedha katika matawi yote likiwemo la Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter