Home BENKI Benki ya wajasiriamali kuanzishwa Zanzibar

Benki ya wajasiriamali kuanzishwa Zanzibar

0 comment 112 views

Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na uvuvi Dk. Makame Ali Ussi amesema kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inatarajia kuanzisha benki ya maendeleo ya wajasiriamali ambayo moja ya kipaumbele chake itakuwa ni kutoa mikopo kwa makundi ya wakulima na wajasiriamali ili waweze kuendeleza shughuli zao na kuchangia katika pato la taifa. Benki hiyo inategemewa kuanzishwa pale itakapokidhi vigezo vya Benki kuu ya Tanzania (BoT)

“Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha taasisi ya fedha kutoa mikopo kwa wajasiriamali lakini huwezi kuanzisha benki kama hujapata kibali kutoka BoT”. Amesema Naibu huyo.

Naibu Waziri Ussi ameongeza kuwa hadi sasa serikali ipo bega kwa bega na taasisi nyingine za kifedha kama  Benki ya Maendeleo yaKilimo Tanzania (TADB) ambayo imekuwa ikitoa mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali wanaojihusisha na kilimo. Aidha, benki ya NMB nayo imeshafanya mazungumzo kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kisiwani humo.

Dk. Ussi ametaja sababu inayokwamisha wajasiliamali wengi kuchukua au kupata mikopo kuwa ni masharti magumu yanayowekwa na taasisi za kifedha kama benki. hivyo kuwafanya wakulima wengi kuwa waoga wa mikopo.

“Wakulima wetu wameanza kufaidika na mikopo inayotolewa na TADB ingawa tatizo wakulima huwa hawapendi kuchukua mikopo”. Amesema Naibu Waziri huyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter