Home BIASHARA Dk. Kijaji apongeza mradi wa soko

Dk. Kijaji apongeza mradi wa soko

0 comment 106 views

Kutokana na  ziara ambazo amekuwa akizifanya, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Ashatu Kijaji kwa ajili ya kukagua maendeleo ya miradi ya kimkakati nchini. Naibu huyo amefurahishwa na jitihada zilizofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Morogoro katika ujenzi wa soko la kisasa ambapo hadi sasa soko hilo limeshakamilika asilimia 30 kati ya 40.

“Ukilinganisha na miradi mingine ya kimkakati niliyoikagua katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, huu ni wa mfano. Ziko halmashauri zilipewa fedha halafu zinarudi tena kuangalia upya mikataba ambayo walitiana saini na serikali jambo ambalo linatia shaka”. Amesema Naibu huyo.

Pia Dk. Kijaji ameutaka uongozi wa Manispaa kukamilisha mradi huo ndani ya miezi mitano ijayo ili wananchi waanze kunufaika ipasavyo.

“Mapato ya soko hili yataongezeka kutoka Shilingi Bilioni moja kwa mwaka hadi shilingi bilioni nne, kwa kuwa idadi ya wafanyabiashara itaongezeka kutoka 400 kwa sasa hadi 900 na huduma nyingine kama benki zitatolewa” amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Regina Chonjo, amefurahishwa na mradi huo kwani anaamini kupitia mradi huo changamoto ya miundombinu haitokuwepo tena na magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu yataisha hivyo afya za wafanyabiashara wa soko hilo kuwa salama.

Kwa upande wake Meya wa manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga, amesema wanategemea kukamilisha mradi huo Septemba mwaka huu na hivyo wafanyabiashara walioondolewa watarudi kuendelea na shughuli zao pale watakapokabidhi mradi.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter