Home BENKI BoT yakagua maduka ya fedha, yatoa tamko

BoT yakagua maduka ya fedha, yatoa tamko

0 comment 150 views

Baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kufanya ukaguzi kwenye maduka ya kubadilisha fedha za kigeni jijini Dar es salaam, imebainika kuwa asilimia kubwa ya maduka hayo yanafanya biashara bila kuzingatia kanuni na taratibu za utoaji wa huduma hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, BoT imeanza mchakato wa kufutia leseni maduka yote yaliyogundulika kuendesha biashara hiyo bila kuzingatia masharti ya leseni.

Mwezi Desemba mwaka jana, BoT iliendesha ukaguzi katika maduka ya kubadili fedha nchi nzima na iligundulika kuwa mengi yalikuwa yakiendesha biashara bila kufuaa Sheria. Baada ya zoezi hilo, Benki Kuu iliagiza maduka hayo kutoa maelezo kwa nini yasifutiwe leseni kutokana na uendeshaji wao wa biashara. Taarifa iliyotolewa imeeleza kuwa, hatua zilizochukuliwa jana zinatokana na tathmini ya taarifa ambazo Benki Kuu ilizipokea kutoka kwa waendeshaji.

BoT imeendelea kusisitiza wananchi kutotumia huduma za kubadilisha fedha zisizo rasmi ili kuepukana na hatari mbalimbali, ikiwemo wizi na kupatiwa fedha bandia.

“Utumiaji wa huduma zisizo rasmi ni kinyume cha Sheria za nchi, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watoaji na watumiaji wa huduma zisizo halali (black market)”. Imesema taarifa hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter