Home FEDHA Uswisi yamwaga mabilioni nchini

Uswisi yamwaga mabilioni nchini

0 comment 113 views

Balozi wa Uswisi hapa nchini, Florence Mattli amesema ubalozi huo kupitia Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC) unatarajia kutoa Sh. 18 bilioni kwa muda wa miaka minne ijayo, kwa lengo la kuwezesha baadhi ya asasi za kiraia zikiwemo Policy Forum, Twaweza na Foundation for Civil Society (FCS) kuimarisha utendaji kazi pamoja na uwajibikaji ili kuimarisha huduma wanazotoa kwa wananchi.

Mattli ameeleza hayo jijini Dodoma na kuongeza kuwa, Uswisi inaamini asasi za kiraia zina mchango mkubwa katika kuiwezesha Tanzania kufikia malengo yake ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 hivyo fedha hizo zitasaidia kukuza uwajibikaji katika mamlaka mbalimbali na kuboresha usimamizi wa sera za maendeleo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze amesema msaada huo utasaidia taasisi hizo kuendeleza ushirikiano uliopo baina yao na serikali.

“Asasi nyingi za kiraia zina mawazo mazuri lakini hazina uwezo wa kuwasilisha mawazo hayo kwenye ngazi husika, msaada huu utatusaidia kuwafikia na kuwawezesha kuwasilisha mawazo ya wananchi”. Amesema Eyakuze.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter