Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Kodi, mikataba halali vyasisitizwa Dodoma

Kodi, mikataba halali vyasisitizwa Dodoma

0 comment 96 views

Licha ya kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa ulipaji kodi na umiliki wa mikataba halali wa upangaji katika masoko ya Halmashauri ya jiji la Dodoma, Ofisa Masoko wa jiji hilo, James Yuna ameendelea kuwasisitiza wafanyabiashara kulipa kodi ya pango kwa ajili ya vibanda vyao ili kuepuka athari za kufungiwa biashara zao.

“Kumekuwepo na mwitikio mkubwa kati ya wafanyabiashara na jiji katika ulipaji kodi na ujazaji wa mikataba halali, hii ni kutokana na elimu inayoendelea kutolewa hadi sasa kwa wafanayabiashara wote husika”. Ameeleza Yuna.

Pamoja na hayo, pia amewataka wafanyabiashara jijini humo kuacha kufanya biashara katika maeneo wanayokatazwa hususani barabara kwani kufanya hivyo kunakwamisha matumizi mengine ya miundombinu kama watembea miguu na vyombo vya moto kupata shida ya barabara. Aidha, ameongeza kuwa kuna wafanyabiashara ambao wamekuwa hawalipi madeni ya kodi kwa muda mrefu na hivyo kukwamisha jitihada za serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Ofisa huyo pia ametoa wito kwa viongozi wa kata, masoko na wadau mbalimbali wa maendeleo kuipa ushirikano serikali katika ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vyote.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter