Home FEDHA Mashirika yanayotengeneza hasara yatajwa

Mashirika yanayotengeneza hasara yatajwa

0 comment 114 views

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad amewaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa mashirika 14 ya umma yana matatizo makubwa kifedha na yameleta hasara iliyopelekea madeni kuzidi mitaji yao kwa asilimia 100. Prof. Assad ametaja mashirika hayo kuwa ni Kampuni ya ndege (ATCL), Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Lindi, Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bodi ya Utalii (TTB), Shirika la Majisafi na Maji taka Dar es salaam (Dawasco) na Kampuni ya Maendeleo ya Nishati ya Joto Tanzania (TGDC).

Ametaja mashirika mengine kuwa ni  Baraza la Biashara la Taifa, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza, Kampuni ya Usafirishaji na Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usambazaji Umeme, Kampuni ya simu (TTCL-Pesa), Bodi ya Maziwa Tanzania, na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (Dawasa).

CAG amesema kati ya mashirika hayo 14, mashirika 11 yamekuwa yakiendeshwa kwa hasara kwa muda wa zaidi ya miaka miwili. Baada ya ukaguzi, Prof. Assad amesema wamegundua limbikizo la deni la shilingi bilioni 11.1 linalotokana na mishahara ya watumishi katika mamlaka za serikali za mitaa zipatazo 22.

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter