Home VIWANDANISHATI Agizo la Kalemani kwa TANESCO

Agizo la Kalemani kwa TANESCO

0 comment 122 views

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dk. Tito Mwinuka kuhakikisha kuwa hadi kufikia Juni 30 mwaka huu, huduma ya umeme inafika katika miji na vijiji vyote vilivyopo hapa nchini. Dk. Kalemani ametoa agizo hilo jijini Dodoma kwenye ziara yake katika vijiji vya Ntyuka na Mkonze alipokuwa akikagua nyumba na maeneo ambayo bado hayajafikiwa na nishati ya umeme na kusisitiza kuwa hakuna sababu ya wananchi kutumia Solar (umeme wa jua) wakati wana uwezo wa kuunganishiwa umeme.

Waziri huyo ametoa wito kwa TANESCO kuacha tabia ya kukataa fedha za wananchi wanaotaka kuwekewa nguzo ili kupata umeme na kusisitiza kuwa wanatakiwa kupokea fedha hizo na kutumiza wajibu wao wa kuunganisha nguzo badala ya kukwepa kazi hizo. Pamoja na hayo amewataka wananchi kutandaza nyaya wakati wanasubiri kuwekewa umeme.

Akiwa Vwawa mkoani Songwe mwezi Desemba mwaka jana, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga alisema kuwa kupitia mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu, hakuna kijiji kitakachoachwa bila umeme kwani serikali imetenga Sh. 1 trilioni maalum kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa na nishati hiyo, wakati ambapo zoezi la uwekaji wa umeme katika vijiji zaidi ya 13,400 likiendelea.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter