Home BIASHARA Airbnb inalipa

Airbnb inalipa

0 comment 123 views

Biashara ya Airbnb inaendelea kukua kwa kasi nchini. Ripoti iliyofanywa na Airbnb kuhusu biashara hiyo barani Afrika mwaka jana inaeleza kuwa Tanzania inashika nafasi ya nne huku na kwamba watu zaidi ya 2,300 wanafanya biashara hii na kujipatia fedha za kimarekani zaidi ya Dola milioni 2.1.

Airbnb ni nini?

Ni kampuni ambayo inapatikana mtandaoni ambayo humuunganisha mtalii au mgeni wa nchi nyingine kuweza kupanga katika nyumba au chumba cha mtu binafsi mara nyingi kwa muda usiozidi mwezi kwa bei nafuu kuliko bei za hotelini ambazo mara nyingi huwa ni kubwa. Kampuni hiyo huchukua kamisheni ya 3% kutoka kwa mpangishaji na asilimia 6 hadi 12 kwa mgeni.

Kwa ufupi, wageni wengi wanaipenda Airbnb kwa sababu ya bei nafuu, pia ni rahisi kujua maelezo zaidi kuhusu sehemu mbalimbali kuhusu nchi husika kwa mfano: sehemu za kutembelea, migahawa n.k.

Kwa upande wa mpangishaji, anajipatia kipato kwa sababu kuna watu wana vyumba vya ziada na hakuna mtu anayetumia na kuna wengine husafiri sana na kuacha nyumba zao bila mtu hiyo kwa kufanya biashara hii kipato cha ziada hupatikana.

Kuhusu usalama wa biashara hii kwa mpangaji na mpangishaji, kuna mfumo ambao hufuatwa. Kwa mfano kutengeneza akaunti kisha kufuata maelekezo ambayo yanahakikishia usalama wa mpangaji na mpangishaji.

Sheria ya Biashara ya Airbnb Tanzania

Septemba 2018, Mkurugenzi wa Utalii Deograsias Mdamu alieleza katika taarifa iliyotolewa kwa umma kuwa ni kinyume na Sheria kwa watoa huduma hao kuendelea kupokea watalii bila kupata leseni.

Uamuzi huo ulitolewa kutokana na vifungu vya Sheria namba 10, 21, na 31 (1-6) vya Sheria ya Utalii ya mwaka 2008 vinavyomtaka mtu au kampuni yenye nia ya kufanya utalii katika majengo ya kujisajili kwa Mkurugenzi wa Utalii ili kupata leseni ya utalii (Tanzania Tourism Business Licence). Mtanzania anatakiwa kulipa Dola za Marekani 400 kwa mwaka kwa ajili ya leseni hiyo wakati wapangishaji wasio watanzania wanapaswa kulipa Dola 600.

Lengo la serikali ni kuhakikisha wapangaji wanalipa kodi kama watu wengine, na kwa wale watakaokutwa bila leseni hatma yao itakuwa ni kulipa faini isiyopungua milioni 10 au kutumikia kifungo kisichozidi miaka miwili au adhabu zote mbili.

Hadi sasa hakuna mtu ambaye amekamatwa kwa kukosa leseni hiyo lakini kama mtu amehamasika kufanya biashara hii, ni muhimu akafuata Sheria kama inavyoeleza kwani ni biashara ambayo inalipa. Siku zote, fedha za ziada ni jambo zuri kwani zinaweza kusaidia katika shughuli nyingi mbalimbali za kila siku.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter