Home BENKI Waziri Mkuu: Utawala bora muhimu

Waziri Mkuu: Utawala bora muhimu

0 comment 102 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameendelea kuhamasisha utawala bora katika utoaji wa huduma za kibenki hapa nchini. Akiwa jijini Arusha kwenye semina ya wanahisa wa benki ya CRDB, Majaliwa ameeleza kuwa mwaka jana, serikali ililazimika kufunga benki takribani tano zilizofilisika kutokana na kukosa utawala bora na tamaa kwa watumishi, hatua ambayo ilipelekea wanahisa na wananchi wakiokuwa wakitumia benki hizo kupata hasara.

Katika maelezo yake, Waziri Mkuu amesema serikali inaratibu kwa umakini mfumo wa kutoa fedha za kigeni na kueleza kuwa hivi sasa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inakamilisha mchakato wa kufungua maduka ya kimkakati ya kubadilisha fedha za kigeni yaliyofungwa awali ili yaweza kufanya kazi katika maeneo ya kimkakati.

Pamoja na hayo, amewahakikishia wafanyabiashara wa maduka hayo kuwa mara maada ya BoT kukamilisha taratibu zake, maduka hayo yatafunguliwa kwa utaratibu maalum. Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa utawala bora na kutoa wito kwa CRDB kutoa elimu ya mjasiriamali ili wafahamu matumizi sahihi ya fedha zao.

“Sitegemei benki hii kufilisika bali itakuwa mfano kwa mabenki bora yanayozingatia utawala bora, pia wale waliofungiwa kufanya biashara za kubadilisha fedha katika maduka mbalimbali nchini, wasubiri Benki Kuu inafanya utaratibu ikikamilisha yatafunguliwa maduka ya kimkakati katika maeneo mbalimbali nchini”. Ameeleza Waziri Majaliwa.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu ameshauri watanzania kujenga mazoea ya kununua hisa ili kuvuna gawio kila mwaka. Amesisitiza kuwa elimu zaidi inatakiwa kutolewa kuhusu ununuzi wa hisa ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter