Home BENKI Kilio kikubwa wateja wa benki hiki hapa

Kilio kikubwa wateja wa benki hiki hapa

0 comment 109 views

Teknolojia za kisasa na masuala ya digitali yanaendelea kukua duniani, na kila siku katika sekta mbalimbali wateja wamekuwa wakitaka mabadiliko yafanyike ili kuwarahisishia ununuzi wa bidhaa au huduma. Hata katika sekta ya fedha hususani benki, wateja wengi wamekuwa wakitaka kuona mabadiliko yanafanyika ili waweze kufurahia huduma zinazotolewa.

Huduma za benki moja kwa moja hufanyika taratibu, jambo ambalo limewafanya wateja wengi kuamua kutafuta taasisi nyingine za kifedha ili kuweza kupata huduma kwa urahisi, muda wowote, sehemu yoyote kwa kutumia mifumo mbalimbali ya kielektroniki. Hivyo muda umefika kwa benki kujua mambo ambayo wateja wanahitaji ili kuendelea kuwa waaminifu.

Punguzo la bei. Kwa mujibu wa utafiti, 45% ya wateja wa benki wanasema sababu kuu inayowafanya wasiondoke katika benki zao ni kwa sababu wanapata punguzo kwenye manunuzi ya riba. Hivyo hii ni njia yenye nguvu katika sekta yoyote, kwani huleta mafanikio na wateja waaminifu kiurahisi. Hivyo benki zinatakiwa kuwa na punguzo la bei ya riba na huduma zao mbalimbali hasa kwa wateja wa muda mrefu hii itawafanya wateja hao kuwa waaminifu kwani itawafanya waone kuwa watahitaji nguvu kubwa sana kupata huduma hiyo katika benki nyingine, hivyo watabaki kuwa wateja wa benki husika kwa sababu wanapata huduma zaidi ya watu wengine na katika bei ya nafuu.

Mbali na punguzo la bei, taasisis kuwa makini huwaridhisha sana wateja na kuwashawishi kuendelea kutumia huduma husika. Kwa mfano, benki ya CRDB wana programu yao ya wiki ya huduma kwa wateja ambapo wateja hupewa nafasi ya kufika katika tawi la benki hiyo kueleza matatizo yake na kupewa suluhisho au hata kupiga simu na kupata suluhisho. Ni vyema benki zikatengeneza misingi kama hiyo ili kuweza kuendelea mahusiano mazuri sio tu na wateja bali jamii kwa ujumla.

Pia wateja wanahitaji kufikiwa na suluhisho au habari kuhusu huduma kwa haraka, au kupata suluhisho kabla tatizo halijatokea ili kujenga uaminifu kwa taasisi huzika. Mwenendo wa benki kama CRDB, NMB, NBC kutuma ujumbe kwa wateja wao kuhusu huduma au habari yoyote inayowahusu wateja wao ni jambo zuri na linawafanya wateja wengi kujenga uaminifu. Muda mwingine kuwapa kipaumbele wateja wa muda mrefu, mfano kwa kuwafanya wajaribu huduma kabla hazijafikishwa kwa umma huongeza uaminifu zaidi kwa wateja kwenda katika benki.

Miaka mingi iliyopita wazo la kuwa na benki mtandaoni lilikuwa ni ndoto tu lakini hivi sasa watu wanafurahia urahisi wa kufanya miamala kwa kupitia simu, kompyuta nk. Ili kwenda sambamba na wateja benki zinatakiwa kuendelea kutengeneza bidhaa zao na huduma zao katika mfumo wa digitali ili kuhamasisha wateja. Huduma kama Sim banking kutoka CRDB imeonyesha mafanikio makubwa kutokana na urahisishwaji wa huduma.

Kwa ujumla, mahitaji, maoni na malengo ya wateja ni muhimu. Taasisi za fedha zina jukumu la kuhakikisha misingi hiyo inafanywa kwa kuzingatia utandawazi na teknolojia za kisasa, hususani zinazochangamkiwa zaidi na vijana.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter