Vijana wanakosea hapa

0 comment 121 views

Miaka ya 20 ni wakati muhimu sana katika kufanya maamuzi ya kifedha kwa kuwa utakuandaa vizuri kwa ajili ya miaka 30. Huu ni umri ambao ambao vijana hufanya maamuzi mabaya ya kifedha kutokana na kuendekeza tabia ambazo kwa asilimia kubwa huwaumiza wanapotimiza miaka 30 na kuendelea. Ili kuwa na uhakika na maisha yako ya baadae, ni vyema kuepuka tabia hizi kuanzia sasa.

Madeni: Endapo utakuwa na madeni bila kuwa na mbinu mbadala ya kuyalipa, utakuwa katika nafasi mbaya kwani kipato ulichonacho hakijitoshelezi hivyo utashindwa kufanya mambo mengine ya msingi. Hili ni tatizo kubwa kwa vijana wengi kwani madeni ni kikwazo cna maendeleo. Huu ni umri ambao unatakiwa kujenga na sio kubomoa. Kama una madeni fanya kila jitihada uyalipe na kama huna basi ni vizuri kuangalia matumizi yako kwa makini na kuepuka kuwa nayo.

Kuogopa kushindwa: Vijana walio wengi sio wavumilivu na hupenda mafanikio ya papo kwa papo hivyo wanakuwa na uoga wa kujaribu vitu vipya. Uoga wa kuanzisha kitu na kufeli umekuwa kikwazo kikubwa na hii huwavunja moyo na kuwatia hofu vijana kuwa wabunifu na kufanya mambo makubwa. Umri huu ni wakati muafaka kujaribu mambo mbalimbali na kupiga hatua mbele. Ukishindwa jifunze, chukua muda kidogo na kisha jaribu tena.

Kukosa malengo: Bila malengo kuanzia mwanzo, ni vigumu kuwa na muelekeo mzuri baadae. Kama kijana unatakiwa kuwa na malengo yako na kutumia muda huu kufanya kazi, kujifunza na  kupiga hatua. Usiangalie nini ndugu au marafiki zako wanafanya na usikubali wakutatishe tamaa kwa namna yoyote ile. Jipange kwa ajili ya maisha yako ya baadae, jiwekee malengo na yafanyie kazi ili yatimie.

Uwekezaji: Asilimia kubwa ya vijana sio wawekezaji. Wengi huweka fedha zao benki tu, kitu ambacho sio kibaya lakini badala ya kufanya hivyo kwanini usiweke fedha zako sehemu ambayo zinaweza kuleta faida? Ukianza kujifunza masuala ya uwekezaji mapema inakuwa rahisi kujifunza kutoka kwa wengine na kufahamu tangu mwanzo sehemu sahihi za kuweka fedha zako. Badala ya kuziweka tu benki, anza kuwekeza kidogo kidogo.

Kuwa na chanzo kimoja cha mapato: Huu ni muda muafaka wa kujituma zaidi na kuacha kutegemea chanzo kimoja cha kupata fedha. Kama umeajiriwa unaweza kuweka akiba kidogo na kuanzisha biashara ndogo. Kusimamia biashara yako mwenyewe ni fursa nzuri ya kujifunza mambo muhimu kama kujitangaza, kutafuta wateja, kumudu bajeti n.k. Kama upo katika nafasi ya kuanzisha kitu kidogo pembeni, huu ni muda mzuri wa kufanya hivyo. Uwepo wa mitandao ya kijamii umerahisisha sana biashara na unaweza kuingiza kipato kirahisi kupitia mitandao kama Facebook na Instagram.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter