Home FEDHA Unataka chanzo kimoja tu cha mapato?

Unataka chanzo kimoja tu cha mapato?

0 comment 83 views

Hivi umewahi kufikiria kuishi kwa kutegemea 50% ya kipato kimoja? Unahisi maisha yako yangekuwa mazuri au marahisi? Kuna watu wengi wanatamani kuishi nyumbani zaidi na kufanya kazi kidogo huku wakiwa na matumizi madogo ili kuweza kuweka akiba lakini wengi wao wanaona hawawezi kumudu maisha hayo.

Watu huwa wana sababu nyingi zinazowapelekea kutaka kuishi kwa kutegemea 50% ya mapato yao ikiwa ni pamoja na kurahisisha maisha kwani ukiweza kuishi ukitegemea asilimia hamsini ya kipato chako basi unaondoa sintofahamu ya masuala mbalimbali yanayohusu fedha.

Vilevile kujiandaa na ujio wa motto inaweza kuwa ni sababu nyingine inayokufanya uishi kwa kutegemea asilimia 50 ya kipato hicho kwa sababu kwa kufanya hivyo itakurahisishia kuweka akiba zaidi ambayo itasaidia baadae familia ikiongezeka.

Kustaafu mapema ni ndoto ya watu wengi hivyo baadhi ya watu huona ni bora waongeze uzalishaji na kuweka akiba zaidi ili wastaafu mapema na kutimiza ndoto nyingine kama kusafiri nk.

Kama unaishi kwa kutegemea asilimia 50 ya mapato yako au chini ya hapo basi itakuwa rahisi kwako kama mambo mabaya yatatokea kwa mfano punguzo la wafanyakazi, kufukuzwa kazi na mambo mengine ambayo yanaweza kuathiri mtiririko wako wa fedha.

Kuna mambo mengi ambayo mtu anaweza kufanya ili kuishi kwa kutumia kipato kimoja. Baadhi ni kama vile:

Matumizi 

Kila mtu katika familia anatakiwa kuwa katika ukurasa mmoja. Kila mtu anatakiwa kujua na kuelewa matumizi yake yanatakiwa kuwa wapi na katika vipengele tofauti. Jitahidi kupunguza matumizi yasiyo kuwa na umuhimu na kama kuna matumizi ambayo unaweza kufanya mwenyewe au kutafuta njia mbadala basi jaribu kufanya hivyo.

Usiangalie watu wengine

Ikiwa unajaribu kuishi kwa kutegemea kipato kimoja basi ni muhimu kuacha kuishi maisha kwa kuangalia watu wengine wanavyoishi. Kwasababu kila mtu ana kipato, malengo na matumizi tofauti. Kuiga watu wengine wanavyoishi kutaleta ugumu katika bajeti kwa kuwa itakulazimu kutumia fedha zaidi ya zile unazoingiza.

Lipa madeni

Madeni kwa namna moja au nyingine yanaweza kukurudisha nyuma ikiwa unataka kuishi huku ukitegemea sehemu moja ya kujipatia kipato. Hivyo baada ya kulipa madeni yako jitahidi kuepukana nayo ili kuondoa mzigo ambao unaweza kukuelemea na kukurudisha nyuma katika malengo kwa ujumla.

Ongeza mapato

Lengo la kuwa na chanzo kimoja cha mapato ni kupata muda wa kufanya mambo mengine. Ikiwa unatumia muda mwingi katika sehemu hiyo moja ya kipato basi hii si njia sahihi kwako hivyo ikitokea njia nyingine ya kukuongezea kipato basi ifanyie kazi.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter