Home BENKI Sifa 4 za ‘Online Banking’

Sifa 4 za ‘Online Banking’

0 comment 150 views

Mambo mengi yanaendelea kuboreshwa na kurahisishwa ikiwa ni pamoja na masuala ya kuhifadhi fedha. Siku hizi huduma nyingi za kibenki zinapatikana kwa njia za mtandao kwenye vifaa vya kielektroniki kama simu na kompyuta. Ikiwa bado huoni sababu ya kujiunga na benki kwa kupitia mtandao, pitia makala hii kufahamu zaidi.

Sababu za kutumia benki za mtandaoni:

Ada

Benki za mtandaoni zimekuwa zikijitahidi kupunguza ada mbalimbali kwa wateja wao ili kuwahamasisha kuendelea kuweka fedha. Kwa kutumia benki ya mtandaoni, gharama za ada hupungua kwa namna moja au nyingine. Hivyo ikiwa unataka kujiunga na benki yoyte inayopatikana mtandaoni ni vyema kuuliza utaratibu wao kuhusu masuala ya ada kwa wateja.

Viwango vya riba

Mara nyingi benki za kawaida huwa hazilipi wateja wao riba kwa kuwekeza akiba zao. Lakini benki za mtandaoni huwalipa wateja riba zaidi kuliko benki za kawaida. Hivyo kama una mahusiano mazuri na benki ya mtandaoni ni rahisi kupata tuzo za hapa na pale,

Ni rahisi zaidi

Benki za kawaida mara nyingi huwa na muda maalum wa kufungua na kufunga matawi yao lakini katika benki za mitandaoni ni rahisi zaidi kwani zinapatikana muda wote hivyo huduma inapatikana masaa yote.

Uzoefu wa teknolojia

Benki za kawaida huwa na wafanyakazi kwa ajili ya kushugulikia wateja katika upande wa teknolojia. Lakini ni tofauti katika benki za mtandaoni ambako mtumiaji huhitaji kuwa na ujuzi unaomfaa ili kuweza kufanya miamala. Ikiwa unahitaji urahisi wa kupata huduma basi benki za mtandaoni zitakufaa zaidi.

Hurahisisha mahitaji

Kuwa na benki ya mtandaoni huondoa wasiwasi katika kipindi cha kufanya mabadiliko kwa mfano kuhama, kusafiri sehemu ambapo hakuna matawi ya benki. Jambo la muhimu ni kuwa na mtandao katika kifaa unachokitumia kufanya miamala.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter