Rais Samia Suluhu amewataka vijana walioajiriwa katika viwanda mbalimbali kuwa na nidhamu sehemu ya kazi na kuacha uzembe.
Rais Samia ametoa wito huo wakatia akizindua kiwanda cha nguo cha Basra Textiles Mills LTD, kilichopo Chumbani –Zanzibar.
“Tubadilikeni tujue kwamba ajira ndio nguzo yako ya maisha, ajira sio by the way, haswa ukiwa kwenye sekta binafsi, ukizubaa nafasi yako imechukuliwa” amesema Rais Samia
“Kama mlivyosikia nilishawahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Wakati ule tulikuwa na viwanda vidogo vidogo vinajikongoja kufanya kazi pamoja na viwanda vingine. Kesi nyingi nilizokuwa nikipokea ni uzembe, kutokuwa na nidhamu ndani ya sehemu za kazi.”
Pia Rais ametaja wizi kuwa miongoni mwa kesi nyingine alizokuwa akikumbana nazo na kuwataka vijana kuacha tabia hiyo.
“Unatoka shift ulichokizalisha unakipunguza unakificha huko, mkipekuliwa kesi serikalini, mnapekuliwa mnavunjiwa heshima, lakini husemi ulichokificha na kikatolewa ndani ya mwili wako.”
Amewataka vijana kufanya kazi kwa uadilifu, heshima sehemu ya kazi, na kufanya kazi kwa weledi.
“Kile unachokijua kitoe chote kuzalisha ndipo mwajiri atakapofurahiwa na wewe na akakutimizia yale yako ambayo unataka kuyafanya” amesema Rais Samia.
Amewataka waajiri kuwatimizia wafanyakazi haki zao kwa mujibu wa sheria ikiwemo mikataba ya kazi.
Amesema takwimu za mwaka 2021 zinaonyesha kuwa Zanzibar inapokea vitenge, kanga na vikoi vyenye thamani ya bilioni 3161.
“Hizi ni pesa nyingi sana kuzipeleka nje kununua hizo bidhaa. Tukiwezesha vizuri kuzalisha hapa ndani, hii fedha itabaki ndani na tutaitumia kwa mahitaji mengine ya wananchi, hivyo tusimamie viwanda vyetu.” ameeleza Rais.
Soma:
Ni aibu kijana kukaa bila kazi : Rais Samia
Mshikamano kuongeza kasi ya ukuaji uchumi