Home AJIRA Maafisa ugani kuajiriwa Bodi ya Korosho Tanzania

Maafisa ugani kuajiriwa Bodi ya Korosho Tanzania

0 comment 365 views

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameiagiza Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuajiri maafisa ugani ili kuongeza tija ya uzalishaji wa Tasnia ya Zao la Korosho nchini.

Waziri Bashe ametoa maelekezo hayo katika Mkutano wa Tathimini ya Uzalishaji, Ubanguaji na Masoko ya Zao la Korosho kwa Msimu wa 2023/2024 katika ukumbi wa PSSSF, jijini Dodoma Aprili 22, 2024.

Waziri Bashe amesema ili kuongeza tija ya Uzalishaji wa zao la Korosho ameielekeza Bodi ya Korosho Tanzania-CBT kuajiri maafisa ugani nchi nzima kwenye kila kata ili kuweza kuwafikia wakulima kwa muda sahihi ili kutatua changamoto wanazokutana nazo katika uzalishaji na utoaji wa elimu wa mara kwa mara.

Amesema itasaidia kuongeza uzalishaji na kufikia malengo ya uzalishaji wa zao la Korosho kutoka tani 305,000 za hivi sasa hadi kufika tani laki saba (7) kufikia mwaka 2027.

Aidha, Bashe ameiagiza CBT kutangaza tenda ya wazi ili kuweza kununua vifaa mbalimbali vya uchimbaji mabwawa madogomadogo vijijini ili ziweze kuwasaidia wakulima katika kilimo kufika mwezi juni 2025.

Pia katika kikao hicho Bashe ameiagiza Bodi hiyo kuhakikisha wanawafikia wakulima wote ili kuweza kuwasajili na kupata idadi ya wakulima pamoja na idadi ya mikorosho ya wakulima ili kuweza kuwasaidia katika ugawaji wa pembejeo na viuatilifu bila ya upendeleo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter